Baada ya kuondolewa kwenye kesi aliyoisimamia kwa moyo mmoja. Ikiwa imebaki hatua ya mwisho kuelekea ushindi. Aliishia kulazimishwa apokee hundi ya milioni kumi. Ila aligoma na kuishia kuacha kazi moja, akiapa angeendelea na upelelezi kwa kutumia ujuzi wa sheria. Asijue wabaya wale hawakupanga hilo litokee. Ndiyo hapo baada ya kunywa pombe kupunguza mawazo, akaja kuzima na kuamka akiwa kitandani.
Kibaya zaidi pembeni yake kuwa binti mdogo umri chini ya miaka kumi na saba. Akitafakari hilo mlango unafunguliwa kwa nguvu wanaingia watu kadhaa wakiwemo polisi. Inakuja kubainika binti alifariki dunia akiwa hapo kitandani, pia aliingiliwa kimwili na kifo chake kinasemekana kimetokana na dawa za usingizi zilizochanganywa na pombe. Kibaya zaidi ushahidi unamlenga yeye mwenyewe, na kuishia ndani. Waliyoona nia wanajitokeza kumtetea, akiwemo Norbert Kaila na Wakili anayeitwa Grace.
Mwishowe inakuja kubainika makubwa yaliyojificha nyuma ya sakata hilo.