Jiji la Istanbul nchini Uturuki linachafuka, wananchi wanaendelea na maisha ya mengine wasijue kama wamevamiwa. Kundi kubwa la majasusi na makundi ya kihalifu ya namna tofauti yameingia hapo. Wapo waliyoingia kama watalii, wengine kikazi na hata kutembelea jamaa. ila nyuma ya pazia kuna kazi kubwa iliyowaleta hapo. Kila kundi ikitaka kuikamilisha kwa upande wao, wasijali wenzao wangeweza au la. Ilimradi ikitimia tu. Shida yote ilianza baada ya kusambaa habari ya kuwepo mnada wa silaha za maangamizi kwa kasi ya moto wa kifuu.
Makundi mbalimbali yakajikuta yakitaka kuhudhuria kwa namna tofauti. Wapo ambao walitaka kujuana na wengi watanue wigo kimaslahi miongoni mwa wahalifu. Pia wapo waliyotaka kuwajua hao waliyofika na ikiwezekana wafanya operesheni ya kuwadhibiti. Asilimia kubwa wakiwa ni miongoni mwa wa majasusi. Mnada kuna ambao walitaka taarifa iliyokuwa kwa mtu maalum, hawajui habari nyingine. Kuna ambao walitaka tiketi kwa mtu tofauti, wakijua mahali ulipo ila tiketi ndiyo muhimu.
Matokeo ikawa watu hao wawili wanafuatwa na wahalifu hadi majasusi, kila mmoja akigombania. Kumbe kuna hila kubwa nyuma ya pazia.