Wizi mkubwa unafanyika, serikali inajikuta ikituma kimakosa mamilioni ya dola kwenda akaunti tofauti. Pesa ambazo zilitakiwa kulipwa mkandarasi, ajabu akaunti wanakuta tofauti ikimaanisha aliyeandaa hati ile ya malipo ndiye mwenye makosa. Mkandarasi naye anacharuka akitoa majuma mawili alipwe, bila hivyo watakuwa wamevunja mkataba na angewaburuza mahakamani kudai fidia na kazi asifanye. Majuma hayohayo maafisa usalama wanaamua kuweka kikao.
Wanaazimia kumteua mpelelezi mmoja ambaye atahitajika kurudisha pesa na pia kuja na majibu kamili juu ya sakata hilo. Bahati inakuja kumwangukia Norbert, aliyechunguza na kuibua mapya. Usaliti, uhaini, utapeli vyote viliibuliwa. Serikali ilizungukwa na bado ilikaribia kuingizwa ndani ya hasara kubwa.