Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginge - E-book - ePub

Note moyenne 
 SHADRACK KIRIMI - Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginge.
Mwongozo huu ni kitabu ambacho kimeandaliwa kimaksudi kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi, mwalimu na msomi wa fasihi kuelewa na kuchambua kwa kina diwani... Lire la suite
2,99 € E-book - ePub
Vous pouvez lire cet ebook sur les supports de lecture suivants :
Téléchargement immédiat
Dès validation de votre commande
Offrir maintenant
Ou planifier dans votre panier

Résumé

Mwongozo huu ni kitabu ambacho kimeandaliwa kimaksudi kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi, mwalimu na msomi wa fasihi kuelewa na kuchambua kwa kina diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine. Mwongozo huu una sehemu mbili kuu. Kuna sehemu ya uchambuzi wa fani na maudhui na sehemu ya kujitathimini; sehemu hii inajumuisha maswali kadha na majibu yake. Hadithi zote zimeshughulikiwa vilivyo. Hadithi hizi ni pamoja na: Tumbo Lisiloshiba, Mapenzi ya Kifaurongo, Shogake Dada ana Ndevu, Shibe Inatumaliza, Mame Bakari, Masharti ya Kisasa, Ndoto ya Mashaka, Kidege, Nizikeni Papa Hapa, Tulipokutana Tena, Mwalimu Mstaafu, Mtihani wa Maisha, na Mkubwa.
Aidha, vipengelele vikuu vya uchambuzi vimeangaziwa. Vipengele hivi ni pamoja na: ploti/msuko, dhamira, maudhui mbalimbali, mbinu za kisanaa pamoja na tamathali za usemi, sifa za wahusika na uhusika wao. Ili kumpa msomaji uhondo kamili, maswali kielelezo yametolewa. Haya ni maswali pamoja na majibu yanayolenga kutoa dira ya namna maswali katika mtihani yanavyofaa kujibiwa. Kila jibu limetolewa hoja za kuridhirisha kuambatana na mitindo mipya ya utahini pamoja na matarajio ya watahini.
Ni maswali ya kumfikirisha msomaji na wakati huo huo kumpa nyenzo za kukabiliana na maswali mengine. Kuna maswali tumbi nzima yakiwa ni pamoja na yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli kutoka katika hadithi. Ni kitabu ambacho kimeyasahilisha masuala yanayoonekana changamano na tata.

Caractéristiques

  • Date de parution
    28/03/2021
  • Editeur
  • ISBN
    978-1-393-17231-4
  • EAN
    9781393172314
  • Format
    ePub
  • Caractéristiques du format ePub
    • Protection num.
      pas de protection

Avis libraires et clients

Avis audio

Écoutez ce qu'en disent nos libraires !

À propos de l'auteur

Biographie de SHADRACK KIRIMI

Shadrack Kirimi ni msomi, mwandishi na mtafiti wa Isimu na Fasihi ya Kiswahili. Ameandika makala na vitabu vya marudio kwa wanafunzi wa shule za upili vikiwa ni pamoja na Hadubini ya Lugha na Hadubini ya Fasihi na Uchambuzi wa Fasihi. Pia, ana tajriba pana katika utahini na kufundisha katika shule za sekondari.i

Vous aimerez aussi

Derniers produits consultés

2,99 €