Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu - E-book - ePub

Note moyenne 
 SHADRACK KIRIMI - Mwongozo wa Kigogo: Maswali na Majibu.
Mwongozo wa Kigogo ni kitabu ambacho kimetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi, mwalimu na msomi wa fasihi katika kuelewa na kuchambua... Lire la suite
2,99 € E-book - ePub
Vous pouvez lire cet ebook sur les supports de lecture suivants :
Téléchargement immédiat
Dès validation de votre commande
Offrir maintenant
Ou planifier dans votre panier

Résumé

Mwongozo wa Kigogo ni kitabu ambacho kimetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi, mwalimu na msomi wa fasihi katika kuelewa na kuchambua kwa kina tamthlia ya Kigogo. Mwongozo huu una sehemu tatu kuu. Kwanza, ni sehemu inayoshughulikia mtitiriko wa matukio katika kila onyesho na tendo. Sehemu ya pili inazamia uchambuzi wa fani na maudhui nayo ile ya tatu ni sehemu ya kujitathmini. Sehemu hii ya tatu inajumuisha maswali kadha pamoja na majibu yake.
Vipengelele vyote vikuu vya uchambuzi wa tamthlia vimeshughulikiwa kwa mapana. Vipengele hivi ni pamoja na: dhamira, maudhui mbalimbali, mbinu za kisanaa pamoja na tamathali za usemi, mandhari, sifa za wahusika na uhusika wao. Ili kumpa msomaji uhondo kamili, maswali kielelezo yametolewa. Haya ni maswali pamoja na majibu yanayolenga kutoa dira ya namna maswali yanavyofaa kujibiwa na uhakiki kutekelezwa.
Kila jibu limetolewa hoja za kuridhisha kuambatana na mitindo mipya ya utahini pamoja na matarajio ya watahini. Ni maswali ya kumfikirisha msomaji na wakati huo huo kumpa nyenzo za kukabiliana na maswali mengine. Kuna maswali chungu nzima yakiwa ni pamoja na yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli na madai yaliyotolewa katika tamthlia. Ni mwongozo ambao umesukwa ukasukika; ukapikwa ukaiva.

Caractéristiques

  • Date de parution
    31/03/2021
  • Editeur
  • ISBN
    978-1-393-40124-7
  • EAN
    9781393401247
  • Format
    ePub
  • Caractéristiques du format ePub
    • Protection num.
      pas de protection

Avis libraires et clients

Avis audio

Écoutez ce qu'en disent nos libraires !

À propos de l'auteur

Biographie de SHADRACK KIRIMI

Shadrack Kirimi ni msomi, mwandishi na mtafiti wa Kiswahili. Ameandika makala na vitabu vya marudio kwa wanafunzi wa shule za upili vikiwa ni pamoja na Hadubini ya Lugha, Hadubini ya Fasihi, Uchambuzi wa Fasihi, Mwongozo wa Chozi la Heri: Maswali na Majibu, na Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine: Maswali na Majibu. Pia, ana tajriba pana katika utahini na kufundisha katika shule za sekondari.

Vous aimerez aussi

Derniers produits consultés

2,99 €