SOLDES

Jusqu'à -70% sur une sélection d'articles*

Revproketaro

Dernière sortie

MAISHA YA WATU NA WANADAMU ANUWAI KATIKA EDENI YA TANZANIA NA MASHARIKI MWA DUNIA

Kitabu hiki kinahusu historia ya ulimwengu wa kale kuanzia miaka bilioni 4.6 iliyopita, na kuanzia miaka elfu 6 iliyopita hadi sasa. Kitabu hiki kimelenga kutoa masimulizi ya kiutamaduni kuhusiana na ulimwengu huo wa kale ambao ulihusika na Watu na Wanadamu anuwai ambao kuanzia hiyo miaka bilioni 4.6, na miaka elfu 6 iliyopita walianza kuishi katika eneo la Mashariki mwa Pangaea ya kwanza na ya pili ambako kulikuwa na Edeni ambayo katika upande wake wa Mashariki ilioteshwa Bustani ya Edeni katika kipindi cha mwanzoni mwa miaka elfu 6 iliyopita. Eneo la Bustani ya Edeni utefu wake ulianzia longitudo 0 hadi longitudo 180 katika bahari ya Mashariki, na upana wake ulikuwa kutoka latitudo 0 hadi latitudo 22.5 kuelekea upande wa Kaskazini na Kusini mwa Pangaea ya pili kabla ya mwaka wa 2348 KK. Watu na Wanadamu walianza kuishi katika eneo ambalo sasa linaitwa "Bonde la Ngorongoro" katika nchi ya Tanzania ambayo ipo katika Afrika ya Mashariki barani Afrika.
Hadi kufikia miaka milioni 145 katika eneo la Edeni ambalo sasa ni bode kubwa, kulitokea mlima mrefu sana ambako Mungu (Elohim) aliweka ikulu yake ya kwanza ya kidunia na kupelekea mlima huo uliokuwa mrefu kuliko milima yote ya ulimwengu wa wakati huo kuitwa "Mlima wa Mungu" (Oldoinyo le Ngai) ambako Elohim alikanyaga miguu yake katika kilele chake. Kati ya kipindi cha miaka milioni 3.6 na miloni 2.5 mlima huo ulioitwa Mlima wa Mungu ulianza kuporomoka na kuharibika kabisa kutokana na vita iliyosababishwa na Mtu asiyekuwa binadamu ambaye aliitwa Lucifa kutokana na kugeuka kuwa mtawala wa ulimwengu kinyume cha sheria ambapo alitumia ikulu ya kidunia ya Eloi iliyokuwa juu ya Mlima wa Mungu (Oldoinyo le Ngai) kufanya uasi ambapo theluthi nzima ya Watu wasio binadamu walioitwa Malaika walimfuata katika uasi wake. Huyo mtu aliyeitwa Lucifa, katika Mlima huo wa Mungu (Oldoinyo le Ngai) alipowasiliana na Watu walioitwa Wanadamu alijivika umbo la nyoka wa kubwa waliokuwa na sura ya mijusi wakubwa walioitwa Dinosaria ili kuwatia hofu na kuwatawala viumbe hai wengine wa nyakati hizo.
Offrir maintenant
Ou planifier dans votre panier

Les livres de Revproketaro